Kipimo cha Kutolewa kwa Gamma ya Interferon (IGRA)

Kipimo cha kutolewa kwa gamma ya interferon (IGRA) ni kipimo cha damu ili kuona kama mtu ana maambukizo ya Kifua Kikuu (TB). Maambukizo ya TB yanatokea kabla ya ugonjwa wa TB. ​

Maambukizo ya TB (pia yanajulikana kama maambukizo ya TB yanayofichika ama ugonjwa wa TB 'unaolala') yapo unapopata vijidudu vya TB katika mwili wako, lakini havifanyi uwe mgonjwa. Mfumo wako wa kinga wa mwili unazuia vijidudu kusababisha uharibifu wowote. Hakuna dalili za maambukizi ya TB na vijidudu haviwezi kusambaza kwa watu wengine.

Maambukizi ya TB ni tofauti na ugonjwa wa TB ambao upo wakati vijidudu vya TB vinapoamka au kuzidi kwa idadi zao na kusababisha uwe mgonjwa na kuweza kusambaza vijidudu kwa watu wengine. 

Ikiwa kipimo cha IGRA cha damu kinaonyesha una maambukizo ya TB, daktari wako anaweza kuagiza dawa ya kuzuia ugonjwa wa TB.​

Habari zaidi kuhusu maambukizo ya TB zinapatikana hapa: Maambukizo ya TB

​Je, IGRA inafanywaje?

Kipimo cha IGRA ni kipimo cha damu kinachohitaji bomba 4 ndogo za damu. Unaweza kula na kunywa kama kawaida kabla ya kipimo. Kinafanya kazi kwa kupima mwitikio wa kinga ya mwili kwa vijidudu vinavyosababisha TB.

Kabla upate kipimo cha IGRA

Tafadhali umjulishe muuguzi au daktari ikiwa wewe:

  • una magonjwa yoyote yanayopunguza kinga kama vile HIV, saratani, au ugonjwa wa figo
  • unatumia dawa inayoathiri mfumo wako wa kinga kama vile steroids (k.m. prednisone), au tibakemikali (dawa za saratani)
  • una homa (>38° C) au ulikuwa na maambukizo katika mwezi uliopita, kama vile mafua, surua, au maambukizo ya kifua 
  • ulikuwa umepata chanjo yoyote katika mwezi uliopita
  • ulikuwa umepata TB zamani au umegusana na mtu mwenye TB.

Baada ya kupata kipimo cha IGRA

Ikiwa matokeo yako ya IGRA ni chanya, unaweza kuwa ulikutana na au kuvigusana vijidudu vya TB hapo awali. Matokeo hasi ya IGRA yana maana kuwa kuna uwezekano kwamba hujawahi kuvigusana vijidudu vya TB.

Muuguzi wako au daktari ataelezea matokeo na kama unahitaji vipimo vyovyote zaidi au matibabu.

Habari zaidi

Ili kupata maelezo zaidi tembelea Karatasi za ukweli za Kifua Kikuu (TB)​. 

Kupata usaidizi bila malipo katika lugha yako, piga simu kwa Huduma ya Utafsiri na Wakalimani kwa 13 14 50.

Current as at: Thursday 3 April 2025
Contact page owner: Communicable Diseases