Ingawa kunaweza kuwa na mabadiliko kuhusu jinsi huduma zinavyotolewa katika baadhi ya maeneo, wafanyakazi wetu waliojitolea na wenye ujuzi wa hali ya juu wa afya ya akili wako hapa ili ku kuhudumia.
Kipaumbele chetu ni afya na usalama wa jamii yetu. Ni muhimu kwa mtu yeyote anayepata shida ya afya ya akili au wasiwasi wakati wowote kufikia msaada na utunzaji. Tafadhali usichelewe - usaidizi unapatikana ikiwa unauhitaji.
Huduma ya dharura
Ikiwa mtu amejaribu, au yuko katika hatari ya mara moja ya kujaribu kujidhuru mwenyewe au mtu mwingine, piga Sifuri Tatu (000)
Kwa msaada wa lugha
Ikiwa huzungumzi Kiingereza, bado unaweza kupata usaidizi wa dharura kwa njia ya simu 24/7, kupitia
TIS National kwa
131 450.
Ushauri wa dharura, wa afya ya akili 24/7, msaada na utunzaji
Ikiwa mtu ana shida ya afya ya akili, au una wasiwasi kuhusu afya yako au ya mtu mwingine ya akili:
Msaada na huduma za afya ya akili
Iwapo wewe au mtu unayemjua anahitaji usaidizi wa jumla wa afya ya akili, tumia
kitafuta huduma za afya ya akili cha NSW Health ili kupata utunzaji unaofaa, au zungumza na daktari wako wa familia kuhusu usaidizi mwingine unaopatikana.
Usaidizi wa simu pia unapatikana kupitia:
Ushauri wa kiafya
Kwa ushauri wa afya ya jumla bila malipo wakati wowote mchana au usiku, piga
healthdirect kwa
1800 022 222. Muuguzi aliyesajiliwa anaweza kukupa ushauri wa afya na ku kuunganisha na huduma unayohitaji. Translating and Interpreting Services (Huduma za Kutafsiri na Ukalimani) wanapatikana kwa nambari
131 450. Kwa habari zaidi tembelea
Healthcare popote pale.